2 Chronicles 9:13-18

13Uzito wa dhahabu ambayo Sulemani alipokea kwa mwaka ulikuwa talanta 666,
Talanta 666 za dhahabu ni sawa na tani 25.
14 bmbali na mapato yaliyoletwa na wafanyabiashara na wachuuzi. Wafalme wote wa Arabuni na watawala wa nchi wakamletea Sulemani dhahabu na fedha.

15Mfalme Sulemani akatengeneza ngao kubwa 200 kwa dhahabu iliyofuliwa. Kila ngao ilikuwa na dhahabu yenye uzito wa shekeli 600
Shekeli 600 za dhahabu ni sawa na kilo 3.5.
16 dAkatengeneza pia ngao ndogo 300 za dhahabu iliyofuliwa, kila ngao ikiwa na uzito wa mane tatu
Mane tatu za dhahabu ni sawa na kilo 1.7.
za dhahabu. Mfalme akaziweka katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni.

17 fKisha mfalme akatengeneza kiti kikubwa cha kifalme kwa kutumia pembe za ndovu na kukifunika kwa dhahabu safi. 18Kiti hicho kilikuwa na ngazi sita na mahali pa kuwekea miguu vyote vya dhahabu. Pande zote za kiti kulikuwa na mahali pa kuegemeza mikono, na simba wawili wakisimama kando ya hiyo mikono.
Copyright information for SwhKC